Goli la
dakika ya 78 la mshambuliaji wa kilabu ya Miembeni City Ibrahim Abdallah(Mkoko)
limepelekea sare katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya combine ya Rolling
Stone na timu ya Dulla Boys.
![]() |
Nyota wa combine ya wilaya ya mjini akiwa na mchezaji mwezake wa Jang'ombe boys. |
Mchezo huo
wa kirafiki uliofanyika mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku katika dimba la
Amani ulikuwa na ushindani kwa pande zote huku ukishuhudiwa kuhudhuriwa na
washabiki kadhaa uwanjani hapo.
Combine ya
Rolling stone ndio ya kwanza kujipitia goli kupitia kwa
Yakubu Amouri goli ambalo lilikuwa kivutio kwa washabiki waliofika katika uwanja huo kutoka na ustadi wa hali ya juu uliofanya na mlinzi.
Yakubu Amouri goli ambalo lilikuwa kivutio kwa washabiki waliofika katika uwanja huo kutoka na ustadi wa hali ya juu uliofanya na mlinzi.
Kuingia kwa
goli hilo kulipelekea vijana wa Dulla Boys kucharukwa nakujianda magol mnamo
dakika ya 48 na 65 kupitia kwa mshambuliaji wao Simai Ali ambae alikuwa kivutio
katika mchezo huo kutokana nakuipa tabu safu ya ulinzi ya combine ya Rolling
Stone iliyokuwa ikiongozwa na mlinzi wakati wa Miembeni City Abubakary Ame.
Rolling
Stone walipata goli la kusawazisha mnamo dakika ya 78 kupitia kwa mashambuliaji
wa Miembeni City Ibrahim Abdallah.
Akizungumza na
mtanadao huu mara baada ya mchezo huo mshambuliji wa combine ya Rolling Stone
Ibrahim Abdallahameelezea kufurahishwa kwake na kiwango alichoonesha katika
mchezo huo huku akitarajia kufanya mazuri zaidi katika michezo ijayo.
Nae mfungaji
wa magol mawili ya timu ya Dulla Boys Simai Ali amesema mchezo ulikuwa na
upinzani huku akielezea kufurahishwa na aina ya uchezaji walionao wachezaji wa
combine ya Rolling Stone.
Kikosi cha Combine ya
wilaya ya mjini kinatarajiwa kuondo visiwani Zanzibar kuelekea Mbulu Manyara
,Tanzania bara July 4 mwaka huu tayari kwa ajili ya mashindano hayo.
Hongera kocha king kwa kuonyesha uwezo wako wakuchagua vipaji na kuviunganisha pamoja
ReplyDelete