By: Abubakary Hatibu.
Tangu Waziri wa
Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma
awakabidhi Uwanja wa Mao Tse Tung wakandarasi wa Kichina kampuni ya Zhengtar
Group Company Limited kwaajili ya kuujenga kisasa uwanja huo ambao utajengwa
kwa mwaka mmoja na miezi miwili, zoezi hilo la ujenzi litaanza rasmi wiki hii
kuanzia kesho Jumanne kwa mujibu wa wataalamu wanaosimamia zoezi hilo.
Mtandao wa
kisanduzenj.blogspot.com ulimtafuta Mhandisi wa uwanja huo Ali Mbarouk Juma
ambapo ameelezea sababu zilizochelewa kidogo kuanza rasmi ujenzi wa uwanja huo.
Mbarouk amesema sababu
kubwa iliyopelekea kudorora kujengwa uwanja huo ni mvua ambapo walilazimika
kusitisha ujenzi kwa kupisha mvua hizo.
Aidha amesema vikwazo
vyengine vilikuwa ni Vibali vya ujenzi ambavyo kwasasa tayari wameshapata na
muda wowote watabandika bango lao la ujenzi kwenye eneo la uwanja huo.
![]() |
Mchoro unaonesha namna utakavyokuwa uwanja wa Mao Tse Tung baada yakukamilika ujenzi wake. |
“Tulikuwa tunasubiria
mvua zipite ndipo ujenzi uanze rasmi, kwasasa mvua tayari zimeshakata muda
wowote kutoka sasa utaanza rasmi, watakaopita katika eneo la uwanja wa Mao
wataona bango ambalo litaonyesha kuwa pana ujenzi wa uwanja, mana ilikuwa
kikwazo chengine vibali vya ujenzi hatujapata lakini kwasasa mambo yapo fresh
na ujenzi kuanzia wiki hii muda wowote unaanza”. Alisema Mbarouk.
Ujenzi huo utakuwa na
Viwanja viwili vya mpira wa miguu na chengine cha michezo ya ndani kama vile
Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Pete na mengineyo.
Katika Viwanja hivyo
vya Mpira wa Miguu uwanja mmoja utakuwepo upande wa Magharibi ambao utakuwa na
Jukwaa moja litakalochukuwa Mashabiki 1500 waliokaa.
Uwanja mwengine wa
mpira wa miguu utakuwepo upande wa Mashariki ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua
Mashabiki waliokaa 900 katika jukwaa moja ambalo litakuwepo katika Uwanja huo.
Viwanja hivyo vitakuwa
na taa ambazo zitaweza kuwezesha kuchezwa michezo hadi usiku.
Uwanja huo utagharimu
Shilingi Bilioni 12.5 kwa fedha za Tanzania ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China itatoa Shilingi Bilioni 11.5 huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kati ya hizo Bilioni 12.5 ambazo
watalipwa Wakandarasi wa uwanja huo ambao ni Kampuni ya Zhengtar Group Company
Limited ambayo ina uzoefu mkubwa wa kujenga Viwanja wa Michezo.
No comments:
Post a Comment