Monday, 5 June 2017

Tutapigana kwa nguvu zote,kutafuta ushindi nyota Jang'ombe Boys.

Nahodha wa timu ya Jang'ombe Boys Ibrahim Sangular amesema ari na hamasa katika kikosi chao imeongezeka maradufu hali ambayo itapelekea kujenga ari na juhudi zao zote kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa jioni ya leo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Nahodha wa timu ya Jang'ombe Boys Ibrahim Sangular katika moja ya michezo ya ligi kuu soka ya Zanzibar.


Akizungumza na mtandao huo akiwa Tanzania  baada kunakofanyika mashindano ya Sport Pesa Super Cup Nahodha huyo amesema watahakikisha wanapambana kwa kunguvu zao zote ilikuwashinda wapinzani sambamba nakusonga katika hatua inayofuata ya nusu fainal.

Ameongeza kuwa wanajua wapinzani wao wa timu nzuri na iliyokusanya nyota wenye uwezo lakini bidii,jitihada na mashirikiano yatapelekea kufanya vyema katika mchezo wao huo huku wakiwaomba wazanzibar kuwaombea ilikufanya vyema katika mtanange huo unaotarajiwa kuwa na mgumu na  waushindani
Nyota wa Jang'ombe Boys wakipozi katika bango la wadhamini wa mashindano ya Sport Pesa Super Cup.

.
"Unajua mchezo utakuwa mgumu sana na ushindani wa hali ya juu lakini tutapigana kwa juhudi zetu zote kuona tufanya vyema katika mchezo huu ,tunajua wapinzani wetu watakuja na kasi kuona wanatushinda lakini ari iliyopo katika kikosi chetu inananipa imani tutashinda katika mtanange huu la msingi niwaombe ndugu zetu watuombee ilikufanya vyema katika mchezo wetu na Gor Mahia"Alisema Sangular.

Akizungumzia ushiriki wao katika mashindano hayo Sangular amesema kuwa amefurahishwa mno na mualiko huo huku wakiyatumia mashindano hayo kuona vipaji vyao walivyonavyo ilikutafuta fursa yakupata timu zakuchezea nje ya Zanzibar.

Nahodha wa Jang'ombe boys Sangular  akiwa mzigoni


"Katika mashindano hayo pakuwepo na walimu na viongozi wa timu mbali mbali za Tanzania na nje ya Tanzania ,hii ni fursa pekee yakuonesha uwezo wako ilikutoka zaidi kisoka na Ishaalah tutajutuma nakuona vipaji vyetu kwa bidii yote ilikuona na sisi tunapata fursa yakutoka kisoka nakucheza timu kubwa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania"Aliongeza Sangular.

No comments:

Post a Comment