Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania {TFF
}limepeleka maombi kwenye Shirikisho la Soka Duniani { FIFA } kuiomea Zanzibar
kuwa Mwanachama wa Shorikisho hilo.
![]() |
Makamu wa Pili wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiishukuru TFF kwa hatua iliyofikia ya kuiombea Zanzibar uanachama katika Shirikisho la Soka Duniani FIFA. |
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Muandamizi anayeshughulikia ruzuku
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} Derek Murusuri wakati
akiwasilisha salamu za Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi kwa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Derek Murusuri alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
limeshaiandikia Barua rasmi FIFA kuhusu suala hilo lilalosubiriwa na wapenda
soka wa Visiwa vya Zanzibar kuwa na uweo wa kushiriki moja kwa moja michezo ya
Kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho hilo la Dunia.
Alisema mipango inaandaliwa na Uongozi wa juu wa TFF katika
kuhakikisha inaipatia nakala Zanzibar kuthibitisha hatua
zilizokwishachukuliwa na Uongozi huo wa juu wa Soka Tanzania.
Afisa Muandamizi huyo
anayeshughulikia ruzuku wa TFF alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwamba TFF hivi sasa inaendelea na mikakati ya kukusanya Vijana wenye
vipaji kwa lengo la kuwandaa kupitia mashindano mbali mbali ya Kitaifa na
Kikanda kwa kuwaona ili kupata Timu imara itakayokuwa na uwezo wa kushiriki
Kombe la Dunia mwaka 2026.
Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana
na Taasisi zake zinazosimamia michezo pamoja na washirika wa Sekta hiyo kwa
juhudi ilizochukuwa za kuisaidia Timu ya Taifa ya Viwanja wenye umri wa
chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys.
Alisema Timu hiyo kwa kiasi kikubwa imeweza kuipa heshima kubwa
Tanzania kwa kiwango ilichofikia katika mashindano ya hivi karibuni ya kuwania
Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika India kwa kutolewa na Timu ya
Soka ya Niger katika hatua ya Robo Fainali.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi mzima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania kwa hatua uliofikia wa kuisimamia Zanzibar katika maombi hayo.
Balozi Seif alisema Zanzibar imekuwa katika harakati za kutafuta
fursa ya kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Soka Duniani FIFA kwa
kipindi kirefu sasa licha ya vikwazo na changamoto nyingi zilizojitokeza na
kukwaza ucheleweshaji huo.
No comments:
Post a Comment