Tuesday, 6 June 2017

Jang’ombe boys yatupwa nje Sport Pesa Super Cup warudi nyumbani kujiandaa na michezo ya nane boro.



 By: Ibny Khamis

Timu pekee ya Zanzibar iliyokuwa ikishiriki katika mashindano ya Sport Pesa Super Cup Jang’ombe Boys wameaga mashindano hayo baada yakupokea kipigo cha magol 2-0 kutoka kwa timu ya Gor Mahia kutoka nchi Kenya.

Wachezaji wa timu ya Jang'ombe boys wakitoka katika uwanja wa uhuru wakiwa na hudhuni baada yakupokea kipigo cha magol 2-0.


Boys ambao walishiriki mashindano hayo wakiwa timu alikwa wanatarajiwa kurudi visiwani leo hii.

Akizungumza na mtandao huo rais wa timu hiyo Ali Othman amesema wameaga mashindano hayo kwa masikitiko huko akisema vijana wake walipoteza mchezo huo kutokana  na kuishiwa na nguvu.

Ameongeza mashindano yale yameleta heshima na motisha kubwa kwa vijana wake na wanarudi zanzibar kujiandaa na michezo ya hatua ya nane bora yanayotarajiwa kuanza baada ya kumalizika mfungo wa sunna ya sita.

“Unajua mashindano yale yameongeza motisha zaidi kwa vijana wangu na hamu yakuiwakilisha nchi kimataifa imeongezeka tunarudi kujiandaa na mzunguko wa pili ambao unaanza mara tu baada ya mfungo wa sunna ya sita ,tunahitaji nafasi zidi yakuwakilishi hivyo tunaelekeza nguvu zetu katika ligi ya nyumbani “alisema Kibichwa.

Kuhusu kutakiwa kwa mlinzi wao wa kati Ali Humud balii na timu ya Simba rais huyo amesema ni mapema mno kulizungumzia suala hilo lakini ukifika muda wake kila kitu kitawekwa wazi.

"Ibny hakuna kitu cha siri katika soka hili suala kama lipo litakuja juu tu wala usijali tumuombe mungu kama lipo liwe la heri ili kijana wetu atoke zaidi katika soka na sisi boys kila tukiona vijana wetu wanatoka kisoka ndo tunakuwa na furaha "alimaliza kibichwa. 
Nyota wa Jang'ombe Boys waliwakilisha katika mchezo huo ni  Ruga Hasham, Said Ibrahim, Amour Firdaus, Chandika Ibrahim, Ally Sammad, Abdi Kassim ‘Babbi’, Abdallah Rashid/Ali Aboukabar dk79, Makame Khamis, Juma Hafidh, Ali Shekha na Abdallah Hussein.

No comments:

Post a Comment