Kocha mkuu wa timu ya combine ya wilaya ya mjini
Unguja ambayo itashiriki katika michezo ya rolling stone Muhamed Seif King amewataka
wadau wa soka wanaoanzisha mashindano ya ndondo cup kuanzisha michezo hiyo
kipindi ambacho ligi zitakuwa zimemalizika.
Kocha king ameyasema hayo wakati alipokuwa
akizungumza na mtandao huu ambao ulitaka kujua sababu ambayo inamfanya kuwazuia
nyota ambao wapo katika kikosi chake wasishiriki katika mashindano hayo ya
Ndondo Cup kila yanapoanzishwa.
Amesema kuwa mashindano ya Ndondo ni mashindano
mazuri kwani yanaongeza ukomavu kwa wachezaji lakini utaratibu wakuanzishwa
mashindano hayo katika kipindi cha ligi inaendelea ndiko kunakoharibu
mashindano hayo.
“Kwanza nataka nikuambie mimi ni muumini wa
mashindano hayo ya Ndondo kwa sababu ili mchezaji apate ushindani na ukomavu lazima
amepitia katika yale mashindano lakini ligi inaendelea huku mashindano yale
yanaendelea hivyo yanamfanya mchezaji achoke jambo ambalo linapelekea wachezaji
wetu wanachoka mapema “alisema kocha huyo.
Akizungumzia soka la Zanzibar kocha huyo amesema
visiwa hivi vimebarikia vipaji vya soka hususani katika kada ya vijana jambo
ambalo linapelekea kufanya vyema katika mashindano mbalimbali ya vijana ambayo
Zanzibar inashiriki.
Ameongeza kuwa Zanzibar ni brazil ya afrika
mashariki kwa kuzalisha vipaji lakini tatizo la umasikini ambalo linawakabili
vijana wengi wenye vipaji ndilo kunakopelekea kufifia vipaji vyao katika umri
mdogo.
Aidha amesema wanaenda katika mashindano ya Rolling
Stone kutetea taji ambalo walitwaa katika mashindano ambayo yamepita.
No comments:
Post a Comment