Wednesday, 14 June 2017

YANGA YAMSAJILI ‘NINJA’ WA TAIFA YA JANG’OMBE.



Na: Mahmoud Zubeiry ,Dar es salam.
 
YANGA imemtambulisha mchezaji wa kwanza kabisa kumsajili kuelekea msimu ujao, ambaye ni beki Abdallah Hajji Shaibu ‘Ninja’ kutoka Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar.
 
Abdallah Hajji Shaibu ‘Ninja’akisaini mkataba wa miaka miwili katika kilabu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniphace Mkwasa amesema beki huyo aliyeng’ara na timu ya taifa ya Jang’ombe katika kombe la mapinduzi sambamba na ligi kuu soka ya Zanzibar  amesaini mkataba wa miaka miwili.

Mkwasa amesema klabu imejiridhidha juu ya ubora wa beki huyo baada ya kupewa taarifa za awali za mchezaji huyo katika soka ya Zanzibar.

Mkwasa amesema Yanga inaendelea na zoezi la usajili kwa umakini wa hali ya juu, ili kuhakikisha hairudii makosa ya kusajili wachezaji wasio na bidii wanageuka kuwa mzigo baadaye.

Kwa ujumla Mkwasa amesema kwamba wanasajili kulingana na mapendekezo ya benchi la Ufundi, chini ya kocha wao mkuu, Mzambia George Lwandamina. 

Kihistoria Zanzibar imekuwa na rekodi ya kutoa mabeki bora ambao wanakuja kuwika kwenye timu za Bara, mfano Kassim Issa aliyewika Mtibwa Sugar miaka ya 2000, Aggrey Morris anayeng’ara Azam FC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ni Nahodha wa sasa wa Yanga anayecheza na Mzanzibari mwingine katika timu hiyo, Mwinyi Hajji Mngwali.

No comments:

Post a Comment