Wednesday, 14 June 2017

CHANEZA KUTAFUTA VIONGOZI WAPYA.



Chama cha mchezo wa netball Zanzibar (CHANEZA) kimekabiliwa na uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya ambao watakaoongoza chama hicho cha mchezo wa netball kuanzia  2017/2021.


Akizungumza na mtandao huu katibu  anaemaliza muda wake wa chama hicho Saidi Mansabu amesema kamati ya uchaguzi tayari imeshapangwa kinachosubiriwa ni kuratibu timu ili kujua ni nani anaestahiki kupiga kura katika chama hicho.

Ameongeza kuwa tayari chama chao kimekutana na viongozi wa baraza la michezo Zanzibar kutoa baraka za uchaguzi huo sambamba na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar ilikufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi.


Akizitaja nafasi ambazo zitagombaniwa kwa upande wa mawilaya ni katibu,mwenyekiti,mshika fedha pamoja na wajumbe wane huku kwa upande wa taifa nafasi ambazo zitagombania ni mwenyekiti,makamo mwenyekiti,katibu ,msaidizi katibu sambamba na mshika fedha.

Akizitaja sifa za wanastahiki kushiriki katika uchaguzi huo katibu huyo anaemalizia muda wake amesema kuwa mdau yoyote yule wa mchezo wa net ball ambae amefikia elimu ya kidatu cha nne nakuwataka wadau mbali mbali wa mchezo huo kujitokeza kugombania nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment