Chama mchezo wa judo
visiwani Zanzibar kipo katika maandalizi yakufanikisha mashindano ya mchezo huo
yanayojulikana kwa jina na Tanzania wit category ambayo yatafanyika mwishoni
mwa mwezi wa saba katika uwanja wa Judo Amani.
![]() |
Wachezaji wa mchezo wa Judo wakiwa katika maonesho ya mchezo huo. |
Akizungumza na mtandao huu
makamo mwenyekiti wa chama hicho Mohamed Khamis amesema mashindano hayo
yatajumuisha vilabu mbalimbali kutoka Tanzania.
Ameongeza kuwa kwa sasa
wanamichezo wa mchezo hyo kutoka Unguja na Pemba wanaendelea na mazoezi ya
mchezo huo huku akiamini kuwa timu za Zanzibar zinatarajiwa kufanya vyema
katika mashindano hayo.
![]() |
Wachezaji wa mchezo wa Judo wa Zanzibar wakikabidhiwa bendera na makamo mwenyekiti wa baraza Mwalim Khamis. |
Amewataka wadau mbali
mbali wa michezo kujiunga katika mchezo huo sambamba nakuwasaidia vijana ambao
wamejiingiza katika mchezo huo.
![]() |
Wachezaji wa mchezo wa Judo wakiwa katika mashindano ya mchezo huo. |
Akizungumzia changamoto
ambazo wanakabiliana nazo katika kuendesha mashindano mbali mbali ya mchezo huo
makamo mwenyekiti huyo amesema uhaba wa fedha sambamba na kutokuwa na wadhamini
ndiko kunakorejesha nyuma juhudi zao katika kuimarisha mchezo huo.
No comments:
Post a Comment