Kamati tendaji ya chama cha mpira wa miguu visiwani
Zanzibar imekutana na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu soka kupitia fomu za
usajili na uhamisho kwa ajili ya msimu wa 2017-2018.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa habari wa
chama cha mpira wa miguu visiwani hapa Ali Bakar amesema zoezi hilo limekuja
baada yakukamilika kwa zoezi la usajili na uhamisho lililoanza tarehe 17 mwezi
wa saba na kukamilika 17 Agosti nakumalizika kwa mafanikio makubwa.
Amesema kuwa zoezi la upitiaji wa fomu hizo limeenda
vizuri huku madai kadadha yakasikilizwa kutokana na baadhi ya wachezaji
kusajili timu mbili.
Akizungumzia baadhi ya kadhia ambazo zimejadiliwa ni
pamoja na suala la mlinzi wa kati wa Miembeni City ambae amesajiliwa na
Mlandege Abubakary Ame ambapo kamati tendaji imerizishwa na hoja ya Miembeni
City na nyota huyo kuidhinishwa kukipiga katika timu ya Miembeni City.
Sambamba na hayo kamati hiyo pia imesikiliza madai
ya Hassan Seif banda ambae pia ameidhinishwa kukipiga katika timu ya Jang’ombe
Boys.
Aidha Cheupe amewataka viongozi wa vilabu kufanya
maandalizi yaliyo mazuri ilikuifanya ligi kuu kwa mismu wa 2017-2018 iwe ya
ushindani na mvuto wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment