MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Miembeni City Feisal
Riyadh Nado, ameahidi kuibuka mfungaji bora wa michuano ya ligi kuu soka ya
Zanzibar inayotarajiwa kuanza October mwaka huu.
![]() |
Feisal akiwa na rais wa Miembeni City. |
Feisal aliyesaini mkataba wa miaka mitatu ni
miongoni mwa washambuliaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao akitokea
Chukwani United alikofunga mabao 22 msimu uliopita..
Akizungumza na mtandao huu Feisal alisema kuwa
anafuraha kujiunga na Miembeni City na kudai alikuwa na ndoto ya muda mrefu kujiunga
na miamba hiyo ya soka visiwani hapa.
“Kwa kweli nimejipanga kufanya vizuri zaidi kuliko
msimu uliopita, natarajia Mwenyezi Mungu atanijalia kila mechi nipate nafasi
yakucheza, niweze kufunga na kuwa mfungaji bora wa ligi,” alisema Feisal.
Mshambuliaji huyo ambae atacheza kwa mara ya kwanza
katika kikosi cha City , hakusita kuisifia timu hiyo akisema kuwa amefurahishwa
na namna inavyojali wachezaji wake.
“Kufika Miembeni City ni njia moja ya mimi kusonga
mbele, hivyo nina mpango wa kucheza soka la kulipwa katika timu kubwa zaidi,
ila hauwezi kwenda kucheza huko bila kujituma mazoezini pamoja na kwenye mechi,
nina imani nitafika huko,” alisema.
Feisal ambaye anavutiwa na staa wa Real Madrid na
timu ya taifa ya Ureno ,Cristiano Ronaldo, amewapa ahadi mashabiki wa Miembeni
City kuwa timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao huku akiwaoamba waisapoti zaidi
timu hiyo.
Hivi sasa straika huyo hatari mwenye spidi na uwezo
wa kupachika mabao, ameshacheza mchezo mmoja na Miembeni City nakuifungutia
timu yake hiyo mpya goli moja katika ushindi wa magol 3-0 dhidi ya mchangani.
No comments:
Post a Comment