Kamati inayosimamia mashindano ya vijana ndani ya
wilaya ya mjini Unguja imejipanga kuona wanazifanyia kazi changamoto
zilizojitokeza katika mashindano ya msimu uliopita ili zisijirejee tena katika
msimu mpya wa mashindano hayo.
Hayo yameelezwa na mshika fedha wa kamati ya
mashindano ya vijana ndani ya wilaya hiyo Mussa Habibu Mzirai wakati alipokuwa
akizungumza na mtandao huu nakusema katika mashindano yaliyomalizika kulikuwa
na kasoro kadhaa ambazo zimepelekea kutia dosori mashindano hayo.
Amesema moja ya changamoto ambazo kamati yake
imekabiliana nazo katika msimu uliopita ni pamoja na vitendo vya upangaji wa
matokeo,mashindano kutokumalizika kwa wakati na uhaba wa viwanja jambo ambalo
kamati yao kwa msimu 2017-2018 itahakikisha changamoto hizo hazijitokeze.
Akizungumzia suala la upangaji wa matokeo Mzirai
amesema vitendo hivyo vilijitokeza mwishoni mwa mashindano ya Central nakuahidi
kutoa adhabu kali kwa yoyote yule atabaaini na vitendo hivyo katika msimu ujao.
Kuhusu zoezi la uhamisho na usajili linaloendelea
amesema zoezi hilo linaenda vizuri huku muamko wa vilabu ukionekana kuwa
mkubwa.
Amewaomba wadau wa wapenzi wa mchezo wa mpira wa
miguu kujitokeza kuunga mkono jitihada za kamati yao ilikuyafanya mashindano
hayo yawe na mvuto na ushindani zaidi.
No comments:
Post a Comment