Kiungo hatari wa timu ya Miembeni City , Haroun Abdallah Jabir(Boban)
ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa mapambano.
![]() |
Kiungo wa Miembeni City Haroun Abdallah Boban. |
Haroun amedai
kuwa moja ya malengo yake ni kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu
soka ya Zanzibar kwa msimu ujao.
“Kuanza kwa msimu mpya 2017-2018, kwangu mimi
nimejipanga kuisaidia timu yangu kuwa mabingwa msimu ujao na mwenyewe kucheza
vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kwani ushirikiano wetu ndio
utatupa hamasa kama wachezaji ya kufanya vizuri na kuisaidia timu yetu kubeba
ndoo (ubingwa),” alisema Haroun wakati
akizungumza na mtandao wa huu.
Haroun ni mmoja wa viungo wanaokuja kwa kasi kwa
sasa Zanzibar, na amekuwa akiwania na vilabu kadhaa visiwani hapa.
Akizungumzia ujio wa Banka ,Guti na Neymar katika kikosi chao Haroun
amesema ujio wa nyota hao kikosini hapo kutasaidia zaidi timu hiyo kufanya
vyema huku akisisitiza kuwa kujituma katika mazoezi sambamba na nakuyafanyia
kazi maelekezo ya mwalimu mchezoni ndiko kutakakoisaidia timu yao hiyo kufanya
vyema katika ligi hiyo.
Sambamba na hayo Haroun amesema kuwa ligi kuu soka
ya Zanzibar ni miongoni mwa ligi ngumu dunia kwa vile inashusha timu nyingi ukilinganisha na idadi ya timu shiriki hivyo inahitajia wachezaji wa timu yao kulijua hilo nakujituma
zaidi hasa katika kipindi hiki cha maandalizi.
Miembeni City inaendelea kujinoa kujiandaana msimu
ujao wa ligi ambapo kwa mara ya kwanza kikosi hicho kinashiriki ligi kuu soka
ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment