Monday, 21 August 2017

ZFA WAMLILIA DR. KUKU.

Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa daktari wa mwanzi wa timu ya taifa ya Zanzibar Abdallah Said Mohammed al-maaruf ‘Kuku’, aliefariki dunia Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar.
 
Pichani Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likitolewa Msikiti Maiti, Michenzani baada ya kusaliwa. ( picha ndogo kushoto marehemu Abdalla Said enzi za uhai wake) .Picha kwa msaada wa mtandao wa bin zubery.

Akizungumza na mtandao huu makamo wa rais wa ZFA Pemba  Ali Muhamed amesema chama chao kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha daktari huyo huku akiwataka wote walioguswa na msiba huo kuwa na subra katika kipindi hiki cha msiba.

Amesema marehemu katika uhai wake alijitolea kwa hali na mali katika kuwahudumia wachezaji wanapopata matatizo yanayowafanya wasiendelea na mazoezi.

Ameongeza kuwa marehemu alikuwa akifanya kazi kwa ushirikioano bila yakujali kuwa anapata chochote au hapati bali alikuwa akihakikisha anaitumia taaluma yake ipasavyo.

Aidha chama chao kiungana na familia ya marehemu Abdallah Said katika kipindi hiki cha msiba nakuwaomba wanzazibar kumuombea dunia ili Allah ampokea akiwa miongoni mwa waja wema.


Marehemu amezikwa jana mchana kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, ambapo mazishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Zanzibar wakiwemo wanamichezo, madaktari na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali alizozifanyia kazi ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) akihudumu katika kiwanja cha kufurahisha watoto Kariakoo kilicho chini ya mfuko huo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema Peponi. Amin.


No comments:

Post a Comment