Timu ya
Mfenisini ambayo imepanda ligi daraja la pili taifa Unguja inatarajiwa
kuelekea Tanzania bara kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya
wa ligi.
Kwa mujibu
wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata timu hiyo itakapokuwa Tanzania bara
itacheza michezo kadhaa yakirafiki yakujipima nguvu ilikukieka sawa kikosi
hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Mwalimu msaidizi
wa timu hiyo Saha ameuambia mtandao huu kwamba baada yakukamilisha kwa usajili
wa nyota wapya wa kikosi hicho kinachofata nikukiandaa kikosi chao hicho kwa
ajili ya msimu mpya wa ligi ambapo timu itashiriki kwa mara ya kwanza.
Amewataka washabiki
na wapenzi wa timu yao hiyo kuwaunga mkono ilikufanya vyema katika msimu mpya
wa ligi nakuweza kupanda daraja.
No comments:
Post a Comment