Mlinzi wa
kati mpya wa timu ya Miembeni City inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar Khalid Boffu aliesajiliwa akitokea Academy ya
Twalipo anatarajiwa kuwasili asubuhi ya kesho akitokea Dar es salam tayari
kujiunga na timu yake kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
![]() |
Halid Boffu akijifua katika fukwe za bahari Boffu atajiunga na wenzake mwishoni mwa wiki hii. |
Khalid ambae
ni mdogo wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya JKU Ruvu Sele Boffu anatarajiwa
kuwasili visiwani mnamo majira ya saa tatu asubuhi kwa boti za Azam Marine.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatika kutoka kwa
uongozi wa timu hiyo atakapowasili visiwani hapa nyota huyo atapokelewa na rais
wa timu hiyo sambamba na viongozi mbali mbali wa timu na natarajiwa kujiunga
katika mazoezi na wenzake kesho kutwa.
Miembeni
City tayari imeanza maandalizi kwa ajili yakujindaa na ligi kuu soka ya Zanzibar
kwa msimu 2017-2018.
No comments:
Post a Comment