Thursday, 22 June 2017

JKU YAHAHA KUTAKA HUDUMA YA BOBAN.

Timu ya JKU inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imepania kuona wanapata huduma ya kiungo mshambuliji wa Miembeni City HarounAbdallah Jabir(Boban).
 
Kiungo anefukuziwa na timu ya JKU Haroun Abdallah Jabir(Boban)
Boban ambae alikuwa chachu ya mafanikio ya timu yake katika msimu uliomalizika wa ligi timu ikiwa inashiriki ligi daraja la kwanza taifa  nakufanikiwa kuipandisha ligi kuu amekuwa akifuatiliwa na timu hiyo kwa kipindi kirefu sasa.

Akizungumza na mtandao huu katibu wa JKU Saad Ujudi amesema mwalimu amependekeza jina la nyota huyo tokea msimu uliopita lakini jitihada zakunasa saini ya nyota huyo ikashindikana lakini bado wanahitaji huduma ya nyota huyo.
 
Kiungo wa miembeni City ,Haroun Abdallah Jabir(Boban) 
Ameongeza kuwa bench la ufundi la timu yake wamependekeza tena jina la nyota huyo kujumuishwa katika usajili wa msimu ujao wa ligi na tayari wameshatumwa watu kufuatilia suala hilo kwa hatua ya awali.

“Tulimuhitaji nyota huyu tokea msimu uliopita lakini ilishindikana kutokana na kuhitajika na timu yake,na msimu huu pia mwalimu aliyopo amependekeza jina lake na sisi kama uongozi tushaanza taratibu za awali zakufuatilia uwezokano wa nyota huyo kujiunga na kikosi chetu”Alisema katibu huyo.

Mtandao huu umemtafuta mkurugenzi wa ufundi wa timu ya Miembeni City, Ali Muhammad kujua kuwa tayari kuna ofa yoyote ile kutoka kwa JKU nakusema mpaka sasa hakuna ofa yoyote ile iliyokuja kutoka kwa timu hiyo.
 
Bobani akiwa na jezi ya timu ya Zanzibar ya shule za msingi.
Amefafanua kuwa JKU waliwafata katika msimu ulimalizika kutaka kumchukua nyota huyo lakini hawakufikia makubaliano kutokana na timu kumuhitaji nyota huyo.

Aidha ameweka bayana kuwa timu yao inakaribisha mazungumzo na timu yoyote ile na endapo watafikia makubaliano wapo tayari kumuachia nyota wao yoyote kuenda timu yoyote ile inayomtaka.






No comments:

Post a Comment