Wakiwa katika
kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika July
9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara mabingwa watetezi wa mashindano hayo
Combine ya wilaya ya mjini usiku wa jana wamejitupa katika dimba la Amani
kukipiga mchezo wa kirafiki na timu ya Jang’ombe.
![]() |
Nyota wa combine ya wilaya ya mjini baada yakumalizika kwa mchezo kati ya timu ya Jang'ombe boys na timu hiyo. |
Katika mchezo huo
ambao ulikuwa wakuvutiwa mabingwa hao wamelazimishwa sare yakutokufanga.
Akizungumzia mchezo
huo kocha masaidizi wa timu hiyo Ramadhani Madundo amesema mchezo ulikuwa nzuri na
waushindani huku akifurahishwa na kiwango kilichoonesha na vijana.
![]() |
Wachezaji wa combine ya wilaya ya mjini. |
Kocha huyo ameongeza
kuwa kwa sasa walimu wa timu hiyo hawaangalii ushindi bali
wanachoangalia ni namna gani vijana wao
wanayafanyia kazi yale wanayowaelekeza katika mazoezi.
Amewataka wadau na wapenzi wa soka visiwani kutoka michango yao ya hali na mali ilikufanikisha safari yao hiyo huku wakiamini kuwa vijana hao watakuja na ushindi.
![]() |
Gulion FC. |
Mjini watacheza mchezo
mwengine wa kirafiki leo Alhamis kuanzia saa 10:15 za jioni dhidi ya timu ya
Gulioni ambayo inashiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
No comments:
Post a Comment