Wednesday, 21 June 2017

TUKIWEKEZA KWA VIJANA TUTAPIGA HATUA KIMICHEZO,MKOKO.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya habari utamaduni utalii na michezo,baraza la michezo ,wizara ya elimu na mafunzo ya amali kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu visiwani ZFA vimeshauriwa kuelekeza nguvu zao  katika kusaidia na kuendeleza michezo kwa vijana ilikutengeza taifa lililobora kimichezo.
Mshambuliaji wa Serengeti boys Ibrahim Abdallah Mkoko akiwa katika majukumu ya taifa .

Ushauri huo umetolewa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania ya chini ya miaka 17 Serengeti boys Ibrahim Abdallah(Mkoko) wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa endapo serikali na wadau wakuu wa michezo wataekeza kuanzia chini Zanzibar itatajika kwa michezo kimataifa.

Amesema nchi zote ulimwenguni ambazo zimepiga hatua kimichezo wameekeza kwa vijana jambo ambalo limeweza kuzisaidia nchi hizo kiuchumi.
Baadhi ya vijana wakizanzibar wakionesha uwezo wao wakusakata kabumbu.

Ameongeza kuwa Zanzibar imebahatika kuwa na vijana wengi wenye vipaji katika michezo mbali mbali lakini kutokuwepo kwa sera nzuri yakukuza,kuendeleza na kuimarisha vipaji vya vijana hao ndiko kunakopelekea kudumaa kwa vipaji vya vijana hao.

Amepongeza mpango wa wizara ya elimu wakuwa na mfumo wa mashindano ya elimu bila malipo ambayo husirikisha wanamichezo kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari nakutoa nafasi kwa vijana kuonesha uwezo wao,nakushauri vijana ambao wataonesha vipaji katika michezo hiyo kuendeleza zaidi ilikuepusha kudumaa kwa vipaji walivyo navyo.

“ Huu utaratibu unaofanya na wizara ya elimu wakuandaa haya mashindano ya elimu bila ya malipo ni nzuri lakini uwepo mpango wakukusanywa wale wote wenye uwezo ilikuendelezwa vipaji walivyonavyo ili visije kupotea”Alisema Mkoko.

Kuhusu Zanzibar kupatiwa uwanachama wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Mkoko amesema ni jambo jema na litasaidia kutoa fursa kwa vijana wakizanzibar kujitangaza huku akikiomba chama cha mpira wa miguu visiwani kuanza maandalizi ya mapema kwa timu zake ambazo huenda zikaanza kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na shirikisho hilo.

“Nimefarijika sana Zanzibar kupata uanachama wa shirikisho la soka barani Afrika huu ni wakati wa vijana wa kizanzibar kutangaza vipaji vyao kimataifa jambo la msingi na la umuhimu nikwa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kuanza maandalizi ya timu zake mapema ilikuona wanafanya vyema katika mashindano wakati utakapowadia”Alisema.

Akizungumza malengo yake katika soka Mkoko amesema ndoto zake ni kucheza soka lakulipwa lakini kwa sasa atahakikisha anafanya mazoezi kwa bidii kuona anaisadia timu yake anayochezea kwa sasa.

“Unajua lengo nikucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania lakini ili upate nafasi yakufika huko lazima ufanye bidii katika mazoezi,uwe na nidhamu ya hali ya juu nakujituma katika mashindano,kwa sasa naaendelea kujinoa kwa ajili ya haya mashindano ya Rolling Stone lakini nikirudi huko nitaelekeza nguvu zangu katika timu yangu,unajua msimu uliomalizika sijapata kuitumikia sana kilabu yangu kwa vile nilikuwepo katika kambi ya timu ya taifa lakini msimu huu nitahakikisha naisaidia timu yangu kwa nguvu zangu zote”Alimaliza Mkoko.



No comments:

Post a Comment