Mshambuliaji nyota wa
timu ya Miembeni City,Muhamed Vuai Prince amesema kwa sasa hana mpango wakuhama
katika kikosi hicho huku akielekeza nguvu zake kuitumikia timu hiyo katika
msimu ujao wa ligi.
![]() |
Mshambuliaji wa timu ya Miembeni City ,Muhamed Vuai Prince akiwa katika mizunguko yake katika mitaa ya Vuga mjini Unguja. |
Prince ameyasema hayo
wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa baada yakuisaidia
timu hiyo kupanda ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 kwa sasa
anajipanga kuona anaisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo
watashiriki kwa mara ya kwanza.
“Tulikuwa na msimu
nzuri tumefanikisha kuipandisha timu ligi kuu nashukuru nilikuwa chachu ya
ushindi katika timu yangu kwa sasa najipanga kuona nafanya zaidi kile
nilichokifanya katika msimu uliopita ilikuisadia timu yangu kutwaa ubingwa wa
ligi kuu soka ya Zanzibar katika msimu wa 2017-2018 ambao timu itashiriki kwa
mara ya kwanza”Alisema Prince.
Ameongeza kuwa licha
yakuwepo kwa taarifa kadhaa juu ya nyota huyo kuondoka katika kikosi
hicho,mshambuliaji huyo amesema yeye binafsi huzisikia taarifa hizo kutoka kwa
watu bali hajafanya mazungumzo na timu yoyote huku kwa sasa akili yake akiielekeza
katika kuisadia timu yake hiyo kufanya vyema katika msimu ujao wa ligi.
Amefafanu kuwa mkataba
wake wa Miembeni City umesalia misimu miwili hivyo haoni haja yakufanya
mazungumzo na timu yoyote ile bali lililobakia kwa sasa nikufanya mazoezi kwa
bidii kubwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.
Ameelezea kufurahishwa
kwake na mazingira yaliyopo katika kikosi hicho huku akifurahishwa na mashirikiano
aliyoyapata katika msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho kutoka kwa wachezaji
wenzake sambamba na uongozi wa timu hiyo.
Prince ambae amemaliza
msimu wa ligi 2016-2017 akiwa kinara wakufumania nyavu katika kikosi cha Miembeni
City kumekuwa na taarifa yakutakiawa na vilabu kadhaa visiwani ikiwemo taifa ya
Jang’ombe.
No comments:
Post a Comment