Aliyekuwa kocha
wa timu ya KMKM inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar Ali Bushir Mahmoud
amekishauri chama cha mpira wa miguu visiwani kutumia njia za busara katika
kufanikisha kupatikana kwa timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka kwa msimu ujao
wa ligi.
![]() |
Kocha wa timu ya Mwadui Ali Bushir Mahmoud. |
Bushir ameyasema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa busara kwa
viongozi wa vilabu sambamba na wale wa ZFA inahitajika katika kufanikisha suala
hilo.
Ameongeza kuwa
endapo viongozi wa vilabu sambamba na wale wa ZFA wataeka pembeni masilahi
binafsi nakuangalia zaidi manufaa ya taifa vilabu 12 vitapatikana bila hata ya
malumbano na migogoro.
Kuhusu suala
la vilabu vilivyopanda ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 kocha
huyo amesema si busara vilabu hivyo kuviunganisha na vile vilivyopo ligi kuu
katika msimu uliopita katika mchako wakutafuta timu hizo bali zijumuishwe
kucheza ligi kuu kama kanuni iliyoendesha mashindano inavyosema.
“Mimi nasikia mijadala mingi sana kama kuna ligi ndogo tusubiri tuone kama itakuwepo hiyo ligi ndogo au vilabu na viongozi wa ZFA watakuja na njia nyengine zakupatikana timu 12 mimi binafsi suala
lakuchezwa ligi dogo kwangu sioni kama kuna tatizo sana ila hizi timu kama Miembeni City
na Charawe sambamba na zile mbili za kule Pemba ambazo zimepanda ligi kuu kwa msimu wa 2017-2018 kwa mujibu wa kanuni sioni sababu yakujumusha hapa
,kama watacheza na wenyewe kwa wenyewe waliopanda kutafuta timu mbili zakupanda badala ya
nne nahisi inaweza kuwa njia sahihi lakini kuwacheza na wale waliopo kwenye
ligi si jambo sahihi kwa muono wangu”alisema kocha huyo.
Aidha amewaomba
viongozi wanaongoza soka la Zanzibar kusimamia sheria zinazoongoza soka
nakujaribu kufanya mazungumzo na baadhi ya makampuni ilikuona haja
yakufadhili ligi kuu soka ya visiwani ilikuongeza mvuto na ushindani katika ligi hiyo.
Akizungumzia
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa na timu ya Mwaduwi yaShinyanga kocha
huyo amesema ligi hiyo inaushindani zaidi ukilinganisha na ile ya nyumbani
Zanzibar huku akiongeza kuwa ushindi umeongezekana zaidi kutokana na ufadhili
ambao upo katika ligi yao.
Amefafanua kuwa
tayari ameshafanya mazungumzo na nyota wawili wanaokipiga ligi kuu soka ya
Zanzibar ambapo ni mlinda mlango sambamba na kiungo mkabaji ambapo bado hajataka
kutaja majina ya nyota hao kwa vile mazungumzo kati ya viongozi wa Mwadui na nyota hao bado hayajafanyika.
No comments:
Post a Comment