Chama cha
mpira wa miguu visiwani Zanzibar kinatarajiwa kuandaa kozi ya ukocha wa
magolikipa kozi ambayo inatarajiwa kufanyika Juni ,28 mwaka huu.
![]() |
Mkufunzi wa kozi ya makocha wa makipa Saleh Machupa. |
Akizungumza
na waandishi wa habari msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani Ali Bakar
amesema kozi hiyo ya ukocha wa magolikipa inatarajiwa kuendeshwa na mkufunzi
anaetambuliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF, Saleh Machupa.
Ameongeza kuwa
kozi hiyo itajumuisha makocha wa magolikipa wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu
soka ya Zanzibar,ligi daraja la kwanza taifa na la pili taifa.
Aidha amesema
kuwa katika msimu ujao wa ligi timu ambayo haitakuwa na kocha wa magolikipa
mwenye cheti timu hiyo itaondolewa katika mashindano kulingana na kanuni ambayo
itatumika katika mashindano hayo.
Amefafanua kuwa kozi hizo za makocha wa magolikipa itakuwa ikiendeshwa kila kipindi kutokana na mahitaji yananafasi hizo visiwani
No comments:
Post a Comment