Viongozi wa
vilabu 28 vya soka vinavyoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar vinatarajiwa
kukutoka katika ukumbi wa mikutano uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kujadili
njia ambazo zitatumika kupatikana kwa timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu kwa
msimu wa 2017-2018.
![]() |
Makamo wa rais wa ZFA Ali Muhamed. |
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa chama cha mpira wa miguu Ali Bakar mbele
ya wanahabari imesema viongozi hao wanatarajiwa
kukutana July ,8 mwaka huu.
Cheupe
amesema kuwa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani uliokutana mwezi
mmoja uliopita umebariki msimu ujao wa ligi uwe na timu 12 hivyo kukutana na
vilabu husika ndiko kutakapotoa fursa ya njia gani ambayo itapelekea kupatikana
kwa vilabu vinavyohitajika katika ligi hiyo.
Ameongeza kuwa
maamuzi ambayo yatafikiwa katika mkutano huo wa viongozi wa vilabu ndiyo
yatakayopelekwa katika mkutano mkuu wa chama hicho nakupelekea kupatikana kwa
timu zitakazoshiriki katika michezo hiyo.
No comments:
Post a Comment