Bodi ya wakurugenzi wa timu ya Miembeni City kesho
wanatarajiwa kukutana na nyota wanaokipiga katika kikosi hicho kwa lengo
lakutoa mkono wa Idd kwa nyota wao hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa timu
hiyo Seif Kombo imesema kwamba huo ni utaratibu ambao upo katika kikosi chao
hicho kila ifikapo mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwakusanya nyota
wao hao kwa lengo lakuwapatia fedha ilikujitafutia huduma ambazo zitawasaidia
kwa ajili ya Idd.
Ameongeza kuwa baada ya kikao cha bodi ya
wakurugenzi wa timu hiyo kilichokutana asubuhi ya leo kimekubaliana kutoa fedha
hizo kwa nyota wao ilikufanya nyota hao kuwa na siku njema ya Idd.
“Huu ni utaratibu ambao tumejiekea kuwapatia fedha
nyota wetu kila ifikapo mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ilioneshana
upendo kati ya viongozi wa timu na wachezaji wetu waliopo katika kikosi chetu
hicho”alisema rais huyo.
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao kuelekea
msimu ujao wa ligi rais huyo amesema baada yakumalizika kwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani wataanza maandalizi ya msimu mpya
wa ligi kulingana na maelekezo ya mwalimu wa kikosi chao hicho.
Kuhusu suala la usajili rais huyo amesema mwalimu amependekeza nafasi ambazo zinahitaji
kufanyiwa marekebisho sambamba na wachezaji ambao waache katika kikosi hicho
kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
No comments:
Post a Comment