Kiungo wa
timu ya Jang’ombe boys Ferej Salum(Ozil) amerejea uwanjani baada yakukaa nje
kwa takribani miezi mitatu kuuguza majeraha ya goti.
![]() |
Kiungo Ferej Salum wakati alipokuwa Villa United |
Fereji ambae
amesajiliwa Jang’ombe boys katika kipindi cha dirisha dogo akitokea Villa United
nakushindwa kuitumikia timu yake hiyo mpya katika michezo ya ligi kuu kutokana
na majeraha hayo aliyoyapata katika michezo yakujiandaa na mzunguko wa pili wa
ligi kuu soka ya Zanzibar.
Kiungo huyo
ambae alikuwa majeruhi ameanza kurudi uwanjani katika mchezo wa kirafiki kati
ya timu ya combine ya Rolling Stone na timu yake mchezo ambao umefanyika usiku
wakumkia leo na kuonesha kiwango cha hali ya juu.
Akizungumza na
mtandao huu kiungo huyo ameeleza kuwa anafurahishwa na hali ya afya yake
nakuwaomba wadau na wapenzi wa soka wazidi kumuombea ili hali yake iwe vizuri
zaidi.
![]() |
Ferej Salum akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha Azam B. |
Ameongeza kuwa
baada yakukaa juu kwa takribani miezi mitatu kwa sasa anatahakikisha anafanya
mazoezi ya nguvu ilikurudisha kiwango chake nakuisadia timu yake kutwaa ubingwa
wa ligi kuu soka ya Zanzibar.
Nyota huyo
ambae pia alipitia katika kituo cha soka cha Azam amesema kwa sasa akili yake
yote anaielekeza katika kurejesha kiwango chake nakuachana na kila aina ya
anasa ilikufikia malengo ambayo amejiekea.
No comments:
Post a Comment