Kampuni ya Jomo
International imezindua rasmi mbio zinazojulikana kama Zanzibar Diabetes
Marathon 2017 zitakazofanyika Novemba 18 mwaka huu ambazo zitakuwa sehemu ya
Siku ya Kisukari Duniani.
Kampeni hiyo
ilizinduliwa rasmi katika Uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar katika mkutano na
waandishi wa habari.
Meneja Masoko wa Jomo
International, Nobert Kabendela alisema kampuni hiyo inaandaa mbio hizi kwa
kushirikiana na Chama Cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Chama Cha Watu wenye Kisukari
Zanzibar (DAZ) na Wizara ya Afya.
“Jomo International
pia inaandaa kambi ya matibabu ya awali ya siku nne kuanzia Novemba 10—14
ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri
kwani mbio hizi zinalenga kutoa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna
ya kupambana nao” alisema na kuongeza kuwa licha ya siku ya Kisukari Duniani
kuwa Novemba 14, mbio zitafanyika Novemba 18 ili kuwapa watu wengi zaidi fursa
ya kushiriki kwani itakuwa mwishoni mwa wiki.
Alisema mbio hizi
zitahusisha Kilometa 21, 10, 5, 2 na kilometa 1 kwa watoto wa shule na kuongeza
kuwa taratibu na vituo vya kujisajili vitatangazwa baadaye na kwamba mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi
Dk Ali Mohamed Shein lakini pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa
kushiriki katika moja yam bio hizo.
Kwa mujibu wa Bw.
Kabendela mshindi wa kilometa 21 atapata milioni 2, Mshindi wa pili – Milioni
1,Mshindi wa tatu – 500,00, Mshindi wan nne – 300,000, Mshindi wa tano –
250,000 na Wengine 50 watakaomaliza– elfu kumi kila mmoja na medali.
Kilometa 10:Mshindi wa kwanza- Milioni 1,Mshindi wa
pili - 500,000, Mshindi wa tatu – 400,000, Mshindi
wa nne – 300,000, Mshindi wa tano – 200,000 namedali kwa
50 wengine watakaomaliza.
Kilometa 5: Mshindi wa kwanza – 500,000, Mshindi
wa piili 400,000, Mshindi wa tatu- 300,000,Mshindi wan nne –
200,000, Mshindi wa tano – 100,000 naMedali kwa wengine
50 watakaomaliza.
Kilometa 2: Wagonjwa wa kisukari ambapo kila mmoja atapata
zawadi na watoto watakaoshiriki katika mbio za kilometa moja Watapata zawadi
mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule.
Kabendela alisema ada
ya usajili ni Kilometa 21 Wageni –Tsh 20,000 na
Watanzania- Tsh 10,000 wakati Kilometa 10 Wageni -
20,000 na Watanzania – Tsh 5,000 Kilometa
5 Wageni 20,000 na Watanzania – 2000 Kilometa
2Watanzania – 1000 na Kilometa moja kwa watoto ni 2000 na
kuongeza kuwa baada ya mbio hizo Jomo itafanya bonanza kubwa katika Uwanja wa
Amaan ambapo kiingilio kitakuwa Tsh 5000.
Akizindua mbio hizo,
Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Suleiman Pandu Rweleza aliishukuru Jomo
kwa kuandaa mbio hizo na kuongeza kuwa ugonjwa wa kisukari umekithiri hivi kuna
haja ya wizara ya Afya na taasisi nyingine kuongeza juhudi.
“Michezo ni afya na
nawashukuru sana kwa kuhusisha suala hili la sukari na michezo kwa kuwa ni moja
ya njia za kukabiliana na ugonjwa huu,” alisema huku akiwaomba wazanzibari
wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizi.
Rais wa chama cha
riadha Zanzibar Dk Abdulhakim Cosmas Chasama alisema wao kama chama wamebariki
mbio hizi na watashirikiana na Jomo kwa karibu kuhakikisha zinafanikiwa kwani
wao kama chama wanatambua athari za ugonjwa wa kisukari katika Visiwa vya
Zanzibar na hata Bara.
Naye Katibu wa DAZ,
Dk. Ali Zuberi aliishukuru kampuni ya Jomo International kwa kubuni wazo hili
zuri ambalo litasaidia kueneza ujumbe wa jinsi ya kupambana na ugonjwa huu wa
kisukari.
“Sasa hivi kisukari ni
tishio sio kwa watu wazima tu bali hata kwa watoto wadogo hivi ni muhimu kutoa
elimu ya kutosha ili kuepusha ugonjwa huu kusambaa zaidi,” alisema na kuongeza
kuwa watashiriki kikamilifu katika mbio hizo.
Alitoa wito kwa
mashirika mbali mbali na makampuni wawaunge mkono katika hili kwa namna yoyote
ili waandaaji waweze kulikamilisha kwani ni zoezi ambalo linahitai fedha nyingi
kulifanikisha.
No comments:
Post a Comment