Sunday, 10 September 2017

UHAMIAJI NET BALL WAELEKEA TANZANIA BARA KUTETEA TAJI LAO.

MABINGWA watetezi wa Netiboli Tanzania timu ya Uhamiaji wanaondoka kesho kuelekea Mkoani Moshi kwa ajili ya kushiriki michuano ya klabu  Bingwa Tanzania.

Michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 13-23 mwaka huu, ambapo Uhamiaji wakiwa mabingwa mara  mbili wamejipanga kuhakikisha wanatetea ubingwa wao huo.

Katibu wa michezo  wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Abrahman Karume ameuambia mtandao huu kuwa wanaondoka wakiwa na matumaini kibao ya kutetea ubingwa huo.

Alisema kuwa hilo kwao halina Shaka na kwa uimara wa timu yao anaimani watafanikisha malengo yao.

"Timu yangu naiamini na mwalimu amejitahidi kuifundisha ili iwe timu bora na inatia moyo wachezaji wote wanaonesha mwamko wa kutetea ubingwa huo", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kiujumla maandalizi yapo vizuri na wanakwenda huko kushindana na sio kushiriki.

" Maandalizi yapo vizuri na tumejipanga kiasi ya kwamba tunakwenda kutetea ubingwa wetu na imani tutashinda", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa ni matumaini yake wanakwenda huko kwa ajili ya kupambana ili warudi na kombe na kutawazwa ubingwa kwa mara  ya tatu.

No comments:

Post a Comment