Friday, 1 September 2017

BLACK SAILORS WAIJIA JUU NDANDA WASEMA DUDU BADO NI MALI YAO.

Timu ya Black Sailors inayoshiriki ligi kuu soka ya Zanzibar imeijia juu timu ya Ndanda FC ya Mtwara inayoshiriki ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania bara kwa kumtumia mchezaji wao Majid Khamis Bakar "Dudu" bila ya kufata taratibu za usajili.


Ndanda walimtumia mchezaji huyo katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara mchezo ambao walipokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Azam FC ambapo mchezaji huyo alicheza takribani dakika 75 akiwa amevalia jezi nambari 12 , namba ambayo alikuwa akiitumia akiwa Black Sailors.

Akizungumza na mtandao huu katibu mkuu wa timu ya Blacksalor Issa Hatibu Masiku amesema utaratibu wa uhamisho wa nyota huyo haujafanyika kutoka kwao na nyota huyo amesajiliwa pia katika timu yao.

Amesema mazungumzo ya awali kwa pande hizo mbili yalifanyika lakini makubaliano hayakufikiwa lakini Ndanda wakaamua kumtumia nyota huo bila yakufuata taratibu za uhamisho.

“Unajua tulifanya mazungumzo ya awali na Ndanda lakini lakushangaza taratibu za uhamisho hazijafanyika nyota huyo ameweza kutumika katika mchezo wao dhidi ya Azam”alisema katibu huyo.


Ameongeza kuwa timu yao itafata taratibu kuona wanapatia haki stahiki huku akiviomba vyama vya mpira wa miguu nchini kuzingatia sheria na kanuni zinafatwa katika kipindi cha usajili na uhamisho.

No comments:

Post a Comment