Wednesday, 31 May 2017

HUSSEIN DECO AUNGANA NA MKOKO ROLLING STONE.

Kikosi cha mabingwa  wa mashindano ya vijana ya Rolling Stone kombain ya Mjini Unguja kimezidi kuimarika baada ya kuongezeka kwa kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys na timu ya Kilimani City Assad Juma lengo ikiwa ni kutetea taji walilotwaa katika msimu uliomalizika.
 
KIUNGO WA KILIMANI CITY ASAAD JUMA AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA TAIFA GABON
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwalimu wa timu hiyo Muhammed Seif King amesema ameamua kumuongeza kiungo huyo ilikuimarisha zaidi kikosi chake.
DECO AKIWA MZIGONI


Ukiachia Hussein Deco nyota wengine walioitwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho ni pamoja na mshambuliaji wa Miembeni City ambae pia alikuwepo katika kikosi cha Serengeti boys kilichokuwepo AFCON Ibrahim Abdallah(Imu Mkoko), mlinda mlango wa Miembeni City Aley Ally,mshambuliaji wa Villa United Juma Ali Yussuf “James” na Muharami Khamis “Terra” wa Black Sailors pamoja na Abdul hamid Salum “Ramos” KVZ.

Kikosi cha Mjini Unguja (Mabingwa watetezi) mpaka sasa kina jumla ya nyota 26 wakiwemo walinda mlango Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame Mkadar Koyo (Huru).
KIUNGO WA KILIMANI CITY ASAAD JUMA AKIWA NA MSHAMBULIAJI WA MIEMBENI CITY IBRAHIM ABDALLAH

Wachezaji wa ndani ni Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum “Ramos” (KVZ), Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jan’ombe), Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Shaaban Pandu (Villa United), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys) na Mohd Ridhaa (Villa United).

 
MKOKO MZIGONI

Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Ibrahim Chafu (Villa FC) ,Ibrahim Abdallah(Miembeni Cit),Asaad Juma (Kilimani City)na Juma Ali Yussuf “James” (Villa United).
KOCHA WA COMBINE YA WILAYA YA MJINI MUHAMED SEIF KING AKISALIMIANA NA KOCHA WA ZIMAMOTO  SEIF BAUSI ALIEVAA FULANA CHEUPE

No comments:

Post a Comment