Tuesday, 30 May 2017

VIONGOZI WAPYA BAZA KUPATIKA MWEZI WA SITA.


Chama cha mchezo wa kikapu visiwani Zanzibar kipo katika mipango ya mwisho yakufanikisha uchaguzi mkuu wa chama hicho.
KIKOSI CHA TIMU YA KIKAPU YA AFRICAN MAGIC 


Akizungumza na zenjsport-on line  makamo mwenyekiti wa chama cha mchezo wa mpira wa kikapu Zanzibar Rashid Hamza amesema harakati za kufanikisha uchaguzi huo zinaenda vizuri.
Uwanja_wa_mpira_wa_kikapu


Ameongeza kuwa kwa mujibu wa marekebisho ya katiba ya chama hicho kutakuwa na mapungufu ya baadhi ya nafasi ambapo mwaka huu kutakuwa na nafasi chache sana zakugombania.

 “Unajua tunachosubiri sasa ni kutoka kwa katiba yetu mpya na katika mpya imepunguza idadi ya nafasi za kugombania tofauti na zamani katiba iliyokuwa ikitumika nyuma ilikuwa na nafasi ya makamo mwenyekiti Unguja na Pemba sambamba na naibu katibu Unguja na pemba jambo ambalo katika katiba mpya nafasi hizo hakuna”alisema makamo mwenyekiti huyo.


Aidha amevitaka vilabu kulipia ada ya mwaka kwa baraza la michezo ilikufanikisha kushiriki katika zoezi hilo la uchaguzi.

No comments:

Post a Comment