Timu ya Jang’ombe
boys wanaendelea kujinoa kwa ajili ya mashindano ya Sport pesa super cup
yanayotarajiwa kufanyika Tanzania bara mapema mwezi ujao .
![]() |
KIKOSI CHA TIMU YA JANG'OMBE BOYS KITAKACHOSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SPORT PESA |
Akizungumza na
zenjsport-on line kocha mkuu wa timu hiyo Mahmoud Abdallah Yussuf amesema
vijana wake wapo katika hali nzuri huku akitarajia kufanya vyema zaidi katika
mashindano hayo.
Aidha
maeongeza kuwa vijana wake wapo katika ari kubwa kuona wanafanya vyema katika
michezo hiyo huku akiamini kuwa watafanya vyema katika mashindano hayo.
![]() |
ABDI KASSIM BABI AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA JANG'OMBE BOYS. |
Akizungumzia
wapinzania wake kocha huyo amesema wanawaheshimu sana wapinzani wao na ni timu
nzuri lakini anawaanda wachezaji wake kwa ajili yakupambana.
Kwa upande
wake Abdi Kassim Babi amesema mazoezi yanaenda vizuri atatumia uzoefu alionao
kuona timu inafanya vizuri katika michezo hiyo.
![]() |
ABDI KASSIM BABI AKIWAJIBIKA NJE YA TANZANIA |
Amewataka
wadau na washabiki wa soka visiwani Zanzibar kuunga mkono juhudi za timu yao
ilikufanya vyema nakuijengea heshima Zanzibar kisoka.
No comments:
Post a Comment