Saturday, 27 May 2017

MKOKO ATOA FUNZO KWA VIJANA WA KIZANZIBAR

Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” amewataka vijana wa kizanzibar kujutuma ilikuitumia fursa iliyoipata Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF.

Mkoko ambae amerejea Visiwani Zanzibar akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys” amesema vijana wa kizanzibar wanatakiwa kuitumikia fursa hiyo ipasavyo ilikujiendeleza zaidi kisoka.
Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” akiwa katika majukumu ya taifa na Serengeti boys.

Akizungumza na zenjsport –on line mshambuliji huyo amesema amefurahishwa mno kwa Zanzibar kupata uwanachama wa shirikisho la soka barani Afrika huku akiamini kuwa vijana wengi wa kizanzibar watapata nafasi yakuonesha kiwango chao.

“Unajua uwanachama wa CAF utatoa nafasi kwa vijana wa kizanzibar kushiriki katika mashindano ya kimataifa binafsi nimefurahishwa mno kufuatia kupatiwa unachama huu na ni muda wa vijana wa nyumbani kuvitangaza vipaji vyetu”alisema mkoko.

Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” akiwa katika mazoezi ya kombain ya wilaya ya mjini Unguja kwenye Uwanja wa Amaan kwa kujiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha.


Akizungumzia ushiriki wake katika mashindano ya AFCON Imu amesema mashindano hayo yamemsaidia kujenga uimara na uwezo wa kiwango chake huku akihidfi kuyafanyia kazi yale yote ambayo amejifunza katika mashindano hayo.

“Kushiriki katika mashindano ya AFCON nimejisikia vizuri kwa sababu nimejenga confidence,nimejifunza nini professional wanaishi, unajua kunatofauti kubwa kati ya mashindano yetu haya ambayo tumeyazoea kama copa cocacola na mengine nitajua vipi nikae katika timu yangu”aliongeza Mkoko.

Ibarahim Abdallah ambae kwa sasa anakipiga katika kilabu ya Miembeni City ambayo imepanda kushiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018 amepania kufanya vyema zaidi ilikufikisha malengo yake ya soka.

No comments:

Post a Comment