Mdau wa michezo
visiwani Zanzibar Mohamed Ibrahim “Raza Lee”amewataka wadau mchezo wa mpira wa
miguu visiwani Zanzibar kuungana kwa hali na mali kuwapatia vifaa sambamba
na michango yao timu ya Combine ya wilaya ya mjini
inayotarajiwa kushiriki katika mashindano ya Rolling stone yatakayofanyika kuanza June
29, 2017 hadi July 9, 2017 jijini Arusha.
Akizungumza na
zenjsport-on line mara baada yakukabidhi vifaa hivyo mdau huyo wa michezo
visiwani amesema ipo haja yakuwaunga mkono vijana hao ambao wamepania kurudi na
ushindi katika mashindano hayo.
Ameongeza kuwa endapo
wadau wa soka watatoa michango yao ya hali na mali imani yake vijana hao
watafanya vyema katika mashindano hayo.
Timu ya combine ya
wilaya ya mjini wanakwenda katika mashindano hayo kutetea taji lao walilotwaa
katika mashindano yaliyofanya mwaka jana Arusha Tanzania.
No comments:
Post a Comment