Wednesday, 8 November 2017

UKATA WA FEDHA WAPELEKEA KUOTA MBAWA KWA LIGI KUU YA NET BALL ZANZIBAR.

Hatimae ligi kuu ya netball iliyokuwa ifanyike kisiwani Pemba yaota mbawa kutokana na ukata wa fedha unaovikabili vilabu sambamba na chama cha mchezo huo.


Hayo yameelezwa na katibu wa chama cha mchezo huo Said Ali mansab wakati alipokuwa akizungumza na mtandao huu.

Amesema chama chao kimepokea taarifa kutoka kwa wenzao waliopo Pemba kuwa vilabu vya Pemba havitashiriki katika ligi hiyo nakupelekea viongozi kukutana hapo jana kujadili suala hilo nakutafuta njia ya kufanya ilikupatikana muwakilishi wa Zanzibar katika ligi ya Muungano.


Aidha ameongeza kuwa baada yakukutana chama cha netball Zanzibar kimeamua vlabu vya Unguja kushiriki katika kombe la Muungano sambaba na mashindano ya Afrika mashariki na kati yatakayofanyika mwezi wan ne mwakani.

Akivitaja vilabu vitakavyoshiriki katika ligi hiyo ya Muungano katibu huyo amesema ni pamoja na JKU,Mafunzo,Duma ,KVZ,Zimamoto na Afya.

Amewataka wadu wa mchezo huo kuwaunga mkono ilikuimarisha mchezo huo visiwani hapa.

Ligi kuu ya Muungano kwa mchezo wa Net ball inatarajiwa kufanyika kuanzia November 26 mwaka huu katika kiwanja cha Gymkhana.












No comments:

Post a Comment