Kamati inayosimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi
(Mapinduzi Cup 2018) inaendelea na matayarisho ya michuano hiyo huku timu 10
zinatarajiwa kushiriki msimu huu.
Hayo yameelezwa na katibu wa kamati ya mashindano hayo Khamis
Abdallah Said wakati akizungumza na waandishi wa habari nakusema kuwa licha
yakupata maombi kutoka kwa timu mbali kuhitaji kushiriki katika mashindano hayo
kamati yao imeamua kuwa na timu kumi kutokana na muda.
Ameomgeza kuwa kuna baadhi ya timu zilikuwa tayari kuharamia
kila kitu wao wakihitaji kushiriki tu katika mashindano hayo lakini kamati yao
imeona muda wakuendesha mashindano hayo hautotosha.
Akizitaja timu amabzo zitashiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Azam ambao ni mabingwa watetezi, Simba na Yanga zote ikiwa nikutoka Tanzania bara huku kisiwa cha Unguja kikiwakilishwa na JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang'ombe na Mlandege na kwa upande wa Pemba kikijumuisha timu ya Shaba na Jamhuri na timu moja kutoka nje ya Tanzania bado haijajulikana lakini itatokea Kenya au Uganda.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Disemba na fainali itapigwa Januari 13, 2018.
Wajumbe wa Kamati wanaosimamia Mashindano hayo Mwenyekiti ni Sharifa Khamis, huku Makamo Mwenyekiti Gulam Rashid, Katibu Khamis Abdalla Said huku Wajumbe wakiwa Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai, Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Ravia Idarous Faina, Ali Mohammed, Mohammed Ali Hilali (Tedy) na Juma Mmanga.

No comments:
Post a Comment