Friday, 12 May 2017

JKU,ZIMAMOTO VITANI LEO KESHO NI DABI YA JANG'OMBE


Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar kutafuta muwakilishi wa Zanzibar katika mashindano ya kimataifa inatarajiwa kuanza leo hii Jumamosi ya Mei 13, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika Viwanja viwili tofauti.

Katika dimba la wa Gombani kisiwani Pemba mnamo majira ya saa kumi alasiri Kizimbani inaoneshana kazi na timu ya Okapi huku katika dimba la Amani muda huo huo wa saa 10 za jioni mabingwa wa tetezi wa ligi hiyo timu ya Zimamoto inaoneshana kazi na vinara wa ligi hiyo kanda ya Unguja timu ya JKU.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Zimamoto.

Jumapili ya Mei 14 ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa michezo miwili ambapo katika dimba la Amani kutakuwa na dabi ya Jang'ombe pale ,Jang'ombe boys itakapooneshana kazi na timu ya Taifa ya Jang'ombe mtanange ambao utavurumishwa mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku.

Huku katika uwanja Gombani kisiwani Pemba mnamo majira ya saa  kumi alasiri Mwenge watamenyana na Jamhuri. i


Mashabiki wa Taifa ya Jang'ombe.

Feisal Salum kiungo wa timu ya JKU.

RATIBA YA MZUNGUKO WA KWANZA
Jumamosi 13/5/2017 Kizimbani v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumamosi 13/5/2017 JKU v/s Zimamoto, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 14/5/2017 Mwenge v/s Jamhuri, saa 10:00 Gombani.
Jumapili14/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s Jang’ombe Boys, saa 2:00 usiku Amaan.

MZUNGUKO WA PILI
Jumatano 17/5/2017 Zimamoto v/s Jang’ombe Boys, saa 10:00 Amani.
Jumatano 17/5/2017 Kizimbani v/s Mwenge, saa 10:00 Gombani.
Alhamis 18/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Alhamis 18/5/2017 Jamhuri v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.

MZUNGUKO WA TATU
Jumapili 21/5/2017 Jang’ombe Boys v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 21/5/2017 Mwenge v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumatatu 22/5/2017 Zimamoto v/s Taifa Jang’ombe, saa 10:00 Amaan.
Jumatatu 22/5/2017 Jamhuri v/s Kizimbani, saa 10:00 Gombani.

No comments:

Post a Comment