Ikiwa michezo ya hatua ya nane bora ligi kuu soka ya Zanzibar kutafuta muwakilishi wa Zanzibar kimataifa ikianza vumbi lake jioni ya leo hapo kesho mahasimu wawili wa Jadi timu ya Taifa ya Jang'ombe na Jang'ombe boys watajitupa katika dimba la Amani mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku kuoneshana kazi.
 |
Mashabiki wa timu ya taifa ya Jang'ombe na Jang'ombe boys. |
Ikumbukwe kuwa mahasimu hao wa jadi walikutana wiki mbili zilizopita katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kwa kanda ya Unguja ambapo katika mchezo huo timu ya Jang'ombe boys ikaibuka na ushindi wa gol 1-0 lililofungwa Khamis Mussa .
Mchezo wao kesho unatarajiwa kuwa na ushindani ambapo taifa wakitaka kulipiza kisasi kwa kuwatumia nyota wao waliopo katika kikosi cha huko nao boys wakihitaji kuendeleza ubabe wao kwa taifa katika ligi.
 |
Kikosi cha timu ya Jang'ombe boys. |
 |
Kikosi cha timu ya Taifa ya Jang'ombe.
|
 |
Ratiba kamili ya michezo ya mzunguko wa kwanza michezo ya hatua ya nane bora ligi kuu soka ya Zanzibar. |
No comments:
Post a Comment