Mshambuliaji
wa timu ya Miembeni City aliepo katika kombaini ya wilaya ya mjini Ibrahim
Abdallah(Imu Mkoko)na kiungo wa KVZ Seif Said kila moja ametupia kambani goli
moja katika ushindi wa magol 2-0 dhidi ya timu ya Fire boys katika mchezo wa
fainal ya mashindano hayo uliofanyika katika uwanja wa Julious Nyerere huko
Mbulu Mkoani Manyara.
![]() |
Kikosi cha Combine ya Wilaya ya mjini wakiwa na kikombe walichotwaa. |
Ushindi huo unakuwa ushindi
wa pili mfululizo wa timu ya wilaya ya mjini baada yakutwaa ubingwa huo katika
mashindano yaliyofanyika mwaka jana.
![]() |
Wachezaji wa combine ya Wilaya ya mjini wakishangilia baada ya ushindi wa magol 2-0. |
Mjini ambao
wametwaa ubingwa wa mashindano hayo bila hata yakupoteza mchezo hata mmoja
katika mashindano hayo wanatarajiwa kulakiwa na mamia ya wapenda soka mara
baada yakuwasili visiwani hapa.
No comments:
Post a Comment