Timu ya
taifa ya Jang’ombe imekubali kipigo cha magol 4-1 kutoka kwa timu ya Zimamoto
ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar mchezo uliovurumishwa katika
dimba la Amani mjini Unguja jioni ya leo.
Magoli ya
washindi yamefungwa na Nyange Othman magol 2 na Ibrahim Hamad magoli 2 huku
goli lakufutia machozi la timu ya Taifa likifungwa na Khamis Faki.
Na katika
uwanja wa Gombani kisiwani Pemba timu ya Jamhuri imeibuka na ushindi wa magol 5-0
dhidi ya Kizimbani.
Ligi kuu
soka ya Zanzibar inaendelea kesho ambapo katika kiwanja cha Amani mjini Unguja
JKU itakipiga na Jang’ombe boys huku katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba
Okapi itakipiga na Mwenge.
No comments:
Post a Comment