Kamati tendaji ya chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar imekutana asubuhi ya leo kujadili masuala kadhaa ikiwemo namna yakupatikana kwa mfumo utakaotumika kuendesha ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018.
![]() |
Akizungumza na mtandao huu baada yakukamilika kwa kikao hicho msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani Ali Bakar amesema katika kikao hicho ukiachia suala la usajili na uhamisho kamati imependekeza kukutana na vilabu kupanga mfumo mpya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Amesema ukiachia suala hilo kamati tendaji imelizungumzia suala zima la usajili na uhamisho sambamba nakuvitaka vilabu kulipia ada ya uanachama kwa ramjisi,ada ya mwaka wilayani sambamba na ada ya mashindano huku akisisitiza kuwa kilabu kitakachokuwa ahakijafanya hayo hakitashiriki katika mashindano kwa msimu ujao.
Kuhusu mfumo uliopitishwa na vilabu kisiwani Pemba afisa habari huyo amesema mfumo ule ulikuja baada ya kupatiwa unachama wa kudumu CAF lakini kutokana na taarifa zilizokuja hivi karibuni kamati hiyo imeona umuhimu wakukutana tena na vilabu kutafuta njia mbadala ambayo itasaidia kupata mfumo.
No comments:
Post a Comment