Monday, 7 August 2017

Cheupe awatoa hofu wazanzibar, asema vilabu vya Zanzibar vitaendelea kushiriki mashindano yanayoandaliwa na CAF.

Licha ya Zanzibar kupokwa uanachama na shirikisho la soka barani Afrika (CAF )vilabu vya Zanzibar vitaendelea kushiriki katika mashindano yanayoandaliwa na shirikisho hilo tofauti na wengi walivyokuwa wakifikiria.
Afisa habari wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar Ali Bakar Ali  (Koplo).

Hayo yameelezwa na afisa habari wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar Ali Bakar wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hapo jana katika chumba cha waandishi wa habari uwanja wa amani mjini Unguja.

Amesema kwa mujibu wa barua ambayo imetumwa July,20 kwa rais wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kutoka kwa kaimu katibu wa shirikisho la soka barani Afrika imeeleza kuwa imefuta maamuzi ya mkutano uliofanyika march 16 mwaka huu ambayo nikupewa unachama kamili tu na sivyenginevyo.

Amewataka wadau wa soka na wazanzibar kwa ujumla kuacha kusikiliza maneno ambayo huzagaa miataani nakusikiliza taarifa mabazo zitakuwa zinatolewa na chama cha mpira wa miguu visiwani ilikujiepusha na taarifa ambazo si sahihi.

Wakati huo huo chama cha mpira wa miguu visiwani imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mjumbe wa kamati tendaji ya chama hicho Suleiman Khamis maarufu Kamba ya Mbuzi kilicotoka asubuhi ya August 7 jijini Dar es salam.
Marehemu Suleiman Khamis( Kamba ya Mbuzi) wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati tendaji ya ZFA taifa wakati wa uhai wake 

Akizungumzia taarifa ya msiba huo msemaji wa chama cha mpira wa miguu visiwani Ali Bakar amesema taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu ni kuwa marehemu Suleiman alikua akisumbuliwa na Pressure na Sukari na kabla ya kusafirishwa kupelekwa Hospitali ya Agaghan jijini Dar es salam, pia alilazwa Hospitali kuu ya Chake Chake Kisiwani Pemba.

Amefafanua kuwa , marehemu aliwahi kuwa muamuzi wa mpira wa miguu wakati chama cha mpira wa miguu kikijulikana kama EFOZA, baada ya hapo alifanikiwa kupewa nafasi ya ukatibu mkuu katika timu ya Chipukizi ambayo kwasasa inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar.


Marehemu amezikwa  jana saa 10:00 alaasiri huko kijijini kwao Kengeja kisiwani Pemba. 

No comments:

Post a Comment