Chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar kupitia kwa msemaji
wake Ali Bakar Ali(Cheupe) kimeweka wazi mifumo mipya itakayotumika kwa ajili
ya ligi madaraja mbalimbali yanayosimamia na ZFA taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari afisa habari huyo amesema
mifumo hiyo imekuja baada ya uongozi wa ZFA kukutana na viongozi wa vilabu
vinavyoshiriki madaraja husika nakukubaliana masuala kadhaa ikiweno namna
itakavyoendeshwa mifumo hiyo ya ligi.
Amesema ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia October 1,huku ligi daraja la
kwanza taifa na la pili taifa ikitarajiwa kuanza baada yakuanza kwa msimu mpya
wa ligi kuu soka ya Zanzibar taarifa yakuanza kwake itatolewa hapo baadae.
![]() |
Kiungo Costatinyo Katepa atashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa mara ya kwanza akiwa na Miembeni City. |
Kuhusu ligi kuu soka ya Zanzibar itachezwa kikanda ambapo kila
kanda itakuwa na timu 14 ambapo timu nne za juu kila kanda zitashindana katika
hatua ya nane bora kutafuta nafasi yakuiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya
kilabu bingwa na shirikisho barani Afrika.
Amefafanua kuwa kila kanda zitashuka timu sita nakupanda timu
mbili ambapo kutapelekea msimu wa 2018-2019 kuwa na timu kumi kwa kila kanda.
Kuhusu ligi daraja la kwanza taifa afisa habari huyo amesema
itajumuisha timu 16 ambazo ligi hiyo itachezwa kwa mfumo nyumbani na ugeni
baada ya mfumo wa makundi kama ilivyozooleka hapo awali na tayari vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo
tayari vimeshaorodhesha viwanja vyao vya nyumbani.
Amefafanua kuwa timu sita za chini zitashuka daraja nakucheza
ligi daraja la pili taifa huku timu mbili kutoka daraja la pili taifa zitapanda
daraja la kwanza taifa.
Kuhusu ligi daraja la pili taifa afisa habari huyo amesema ligi
hiyo itakuwa na timu 36 ambapo ligi hiyo itachezwa kwa mfumo wa makundi ambapo
zitapangwa kwenye makundi matatu na kila kundi kushuka timu tatu.
No comments:
Post a Comment