Kocha msaidizi wa timu
ya Unguja itakayoshiriki katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule
za Sekondari Tanzania (UMISSETA) Abdul Wahab Dau ametangaza kikosi cha mwisho kinachojumuisha nyota 21 tayari kwa ajili ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Butimba ,Mwanza June
6, 2017.
Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi kocha huyo amesema katika kikosi hicho wamejaribu kuangalia
uwezo wa wachezaji husika sambamba na nidhamu ya mchezaji.
Kikosi hicho cha timu ya shule ya sekondari Unguja
kinaundwa na walinda mlango Aley Ali
Suleiman (Ubago) na Ali Makame (Muembe ladu)
![]() |
KIKOSI CHA UMISETA |
Huku walinzi wakiwa Ibrahim
Abdallah Hamad (Arahman), Abdurahman Seif Bausi (Glorious), Abubakar Khamis
(Bububu), Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Ali Issa Omar (Lumumba),
Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki) na Abbas Yahya.
Huku viuongo wakiwa Amani
Ali Suleiman (Kiembe Samaki), Ibrahim Faraj “Mess” (Lumumba), Haji
Suleiman (JKU Mtoni), Yakoub Kiparo (Langoni), Jamali Ali Jaku “Ozil” (Kinuni)
na Eliyasa Suleiman (K-pura).
Huku kwa upande wa
washambuliaji Faki Kombo (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan
(Bububu), Walid Abdi “Pato” (Mwera), Ali Mohd Seif (Tumekuja) na Ali Omar
(Mwera).
Kikosi hicho
kinatarajia kuondoka Visiwani Zanzibar siku ya Jumapili June 3, 2017.
No comments:
Post a Comment