Tuesday, 25 April 2017

BABU SHUBE ATOA SOMO KWA WAANDISHI

ALIYEKUWA kocha wa Timu ya Mdungu United Mohamed Shubeir, amesema ni jambo zuri kwa waandishi wa habari za michezo Kisiwani Pemba, kupatiwa taaluma hasa katika kipindi hiki cha Zanzibar kupata uwanachama wa CAF.

Alisema waandishi wa habari sasa wataweza kufanya kazi zao kwa umakini mkubwa, huku akiwataka makocha wenzake kuhakikisha wanatoa

mashirikiano kwa waandishi.

Shubeir aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, katika uwanja wa michezo Gombani baada ya kumalizika kwa
mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya CAF INTERCLUB
MEDIA GUIDELINS 2009.

“Waandishi wa Pemba wamekuwa wakikumbana na changamoto mbali mbali, zaidi kutoka kwa makocha wakati wanapotaka kufanya mahojiano nao, ni
jambo zuri sasa kwa makocha nao kupatiwa taaluma kama hiyo”alisema.

Aidha Shubeir alisema sasa wakati umefika kwa waandishi kuhakikisha
wanabadilika, katika uwandishi wao katika kipindi hiki Zanzibar
iliopata uwanachama wa CAF.

Alisema waandishi wanapaswa kuzisoma na kuzijuwa kwa kina kanuni za
shirikisho hilo, katika mashindano mbali mbali wanayoyasimamia ikiwemo
na ligi za nchi husika ili kuepuka kujakutia doa taifa.


Hata hivyo aliwataka makocha wenzake kubadilika kwa kwenda kufuata
taaluma za ukocha zaidi ili kuwendana na sheria na kanuni za CAF.

No comments:

Post a Comment