Tuesday, 25 April 2017

KHAMIS MUSSA ‘RAIS ‘ AIBEBA BOYS.

Khamis Mussa rais ameendeleza rekodi yake yakuwafunga mahasimu wao wa jadi ya Taifa Jang’ombe baada yakuifungia goli pekee la ushindi katika ushindi wa goli 1-0 mtanange uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja usiku wakuamkia leo.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuhudhuriwa na mashabiki lulkuki uwanjani hapo hadi timu zinaenda mapumziko hakuna timu iliyoona lango la mwenziwe.

Kurudi uwanjani kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko na mabadiliko hayo yaliinufaisha zaidi boys ambao walijiandikia goli hilo mnamo dakika ya 86 kutokana na kazi nzuri iliyofanya na Khamis Mussa.

Akizungumzia mchezo huo kocha msaidizi wa timu ya Jang’ombe boys Issa Amasha amesema mtanange huo ulikuwa nzuri na ushindani kwa pande zote nakuelezea kufurahishwa na ushindi huo.

Aidha kocha huyo amesema kuwa tayari timu yao imetinga katika hatua ya nane bora hivyo maandalizi yao kwa sasa nikuhakikisha timu inafanya vyema katika hatua hiyo nakutwaa ubingwa wa Zanzibar kwa msimu huu wa ligi.

Nae mwalimu wa timu ya taifa ya Jang’ombe Saleh Mussa Maisara amesema mchezo huo ulikuwa na ushindani kwa pande zote mbili lakini kutolewa kwa mchezaji wake kwa kadi nyekundu ndiko kulikopelekea kupoteza mchezo huo.

Aidha ameongeza kuwa wanarudi katika mazoezi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo huo ilikufanya vizuri katika michezo miwili iliyosalia.

Kikosi cha timu ya Jang'ombe boys kilichoanza katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi Taifa ya Jang'ombe



Kikosi cha timu ya Taifa ya Jang'ombe kilichoanza katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi Jang'ombe boys .

No comments:

Post a Comment