Nahodha wa vinara wa mashindano ya hatua ya nne bora ligi daraja la kwanza taifa Unguja timu ya Miembeni City Habibu Ali ameweka wazi kuwa wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ng’ome unaotarajiwa kufanyika May 9 mwaka huu.
Habibu amesema kwamba kikosi hicho kipo vizuri na watanufaika na urejeo wa wachezaji wao muhimu waliokuwa majeruhi, akiwemo nahodha msaidizi Haroun Abdallah Boban na walinzi wao Ahmed Keis na Yussuf.
![]() |
Nahodha wa timu ya Miembeni City Habibu Ally |
‘’Morali iko juu, timu ipo
vizuri bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo
fiti na wako tayari kwa mchezo naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri ya
kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” alisema.
Kiungo huyo anayesifika kwa ukabaji na mwenye mashuti makali, aliongeza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuhitaji usindi katika mchezo huo na tayari wamekutana mara mbili katika msimu huu wa ligi nakutoka sare katika michezo yote miwili.
“Usidhani kama mchezo utakuwa rahisi ,tunawajua wapinzani wetu tumecheza nao mara mbili katika msimu huu nakutoka sare katika michezo yote miwili ,wanakuja na ari na kasi kuona wanashinda ilikufufua matumaini yakusonga mbele,lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisema.
Habibu ambaye amekulia kwenye timu hiyo kwa takribani miaka minne sasa, ametoa wito kwa mashabiki wa Miembeni City kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi uwanjani na kuibuka kidedea.
Miembeni City wanaongeza
mashindano hayo ya hatua ya nne bora baada yakushuka dimbani mara mbili
wakishinda katika michezo yote miwili kwa kuwafunga Charawe 2-0 na Seblen 2-0 wapo
kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo kinaendelea na mazoezi
katika kiwanja cha Amani mjini Unguja kujiandaa na mchezo huo.
No comments:
Post a Comment