Thursday, 4 May 2017

JAMHURI YAJIPANGA KUFANYA VYEMA HATUA YA NANE BORA.



Kocha mkuu wa timu ya Jamhuri Abdulmutik amesema wanajipanga kuona wanafanya vyema katika michezo ya hatua ya nane bora ligi kuu soka ya Zanzibar.

Akizungumza na zenjsport kocha huyo amesema baada yakumaliza ligi kuu kwa kanda ya Pemba wakiwa vinara wa ligi hiyo kocha huyo amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao zote katika hatua ya nane bora ilikuiwakilisha nchi kimataifa.

Ameongeza kuwa ari katika kikosi chake imekuwa ya hali ya juu huku viongozi pamoja na beanch zima la ufundi limeandaa mikakati yakutosha yakuona timu inafanya vizuri katika michezo hiyo ya 8 bora.

Akizungumzia soka katika kisiwani cha Pemba kocha huyo ambao aliwahi kuifundisha timu ya Kijichi amesema katika kisiwa cha Pemba kiwango cha soka kipo cha hali ya juu kinachokosekana ni sapoti kutoka kwa wadau mbali mbali wa soka.



Kocha wa timu ya Jamhuri Abdull Kiduu

No comments:

Post a Comment