Wednesday, 19 April 2017

MAANDALIZI YOTE KUELEKEA MKUTANO MKUU ZFA YAKAMILIKA CHEUPE

Mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar unatarajiwa kufanyika Jumamos ya April 22 katika kisiwa cha Pemba.

Akizungumzia maandalizi ya mkuutano huo mbele ya wanahabari afisa habari wa chama cha mpira wa miguu  visiwani Ali Bakar amesema maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yanaenda vizuri.

Ameongeza kuwa kwa sasa chama chao kipo katika hatua za mwisho zakukalisha utoaji wa posho kwa wajumbe wa mkutano huo waliopo Unguja ili wakamilishe mahitaji muhimu ya familia zao.

Aidha amesema baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wanatarajiwa kuondoka Ijumaa kuelekea kisiwani Pemba kwa usafiri wa baharini huku wengine wakitarajiwa kuondoa Jumamos kupitia usafiri wa angani.

Akizungumzia ajenda za mkutano huo amesema ajenda kuu ya kumtano huo ni mabadiliko ya katiba huku ajenda nyengine ndogondogo zikitarajiwa kujadiliwa katika mkutano.


Mkutano huo mkuu wa zararua unafanyika kufiatia ule uliofanyika katika kisiwa cha Unguja wiki tatu zilizopita unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
AFISA HABARI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU VISIWANI ZANZIBAR ALI BAKAR ALI (CHEUPE)

No comments:

Post a Comment