Sunday, 23 April 2017

SERENGETI BOYS ‘YAWACHAPA’ GABON 2-1 MOROCCO, MKOKO AFUNGA GOLI LA USHINDI.

Mshambuliji wa timu ya Miembeni City Ibrahim Abdallah aliepo katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17 ameendeleza makali yake yakufumania nyavu baada yakuifuaingia timu hiyo goli la ushindi katika ushindi wa magol 2-1 dhidi ya Gabon.

Mshambuliaji wa timu ya Serengeti boys Ibrahim Abdallah (Mkoko) mwenye jezi namba 17 akishangilia goli na kiungo wa Asaad  
Katika mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni miongoni mwa maandalizi ya timu hiyo kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 Mkoko amejipatia goli hilo mnamo dakika ya 75 huku goli la kwanza likifungwa , Kelvin Nashon Naftali dakika ya 18
.

Akizungumza na zenjsport on line mshambuliaji wa timu ya Miembeni City Ibrahim Abdallah ambae yupo katika kambi hiyo ya Serengeti boys ameelezea kufurahishwa kwake na kiwango ambacho ameonesha katika mchezo huo nakusema kuwa anajipanga kuona anafanya vyema katika kila mchezo.

Aidha mshambuliji huyo amewataka wachezaji wenzake wa timu ya Miembeni City ambao wapo katika kambi kujiandaa na mchezo wao wa pili ligi daraja la kwanza taifa Unguja kuongeza bidii ya mazoezi huku akiwata kujutuma kwa nguvu zote nakupandisha timu ligi kuu.

Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.


Huo unakuwa mchezo wa nne wa maandalizi kwa Serengeti kujiandaa fainali za Gabon, baada ya kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.
Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana.

No comments:

Post a Comment