Tuesday, 18 April 2017

MIEMBENI CITY ,YATUMA SALAMU KWA SEBLEN,YAILIPUA CHARAWE 2-0 .

Timu ya Miembeni City imeanza vyema kampeni yake yakutafuta tiketi yakucheza ligi kuu soka ya Zanzibar baada yakuifunga timu ya Charawe magol 2-0 katika mchezo wa hatua ya nne bora mtanange uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja.

Katika mtanange huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote City wamejipatia magol yao kupiti Seif Salum Zola na Muhamed Vuai Prince.

Miembeni City ambayo imeeka kambi katika maeneo ya Fumba wilaya ya magharibi A Unguja itajitupa tena dimbani April 26 kumenyana na Seblem mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kwa pande zote.

Matokeo hayo ya magol 2-0 waliyoyapata Miembeni City wanaendeleza rekodi yake yakutokupoteza katika michezo yake waliyokutana na Charawe ambapo timu hizo zimekutana mara saba Miembeni City wakishinda michezo sita huku wakitoka sare katika mchezo mmoja.
Walinzi wa timu ya Miembeni City Ali Mwinyi na Yussuf baada ya mchezo na Charawe mchezo ambao City imeibuka na ushindi wa magol 2-0.


Wachezaji wa Miembeni City wakiwasalimia washabiki wao kabla yakuanza mchezo kati ya timu yao na timu ya Charawe mchezo ambao City imeibuka na ushindi wa magol 2-0.

Wachezaji wa Miembeni City wakifuatili mchjezo kati ya timu ya Ng'ome na timu ya Seblen mchezo ambao Ng'ome waliibuka na ushindi wa magol 2-1

No comments:

Post a Comment